NAIBU waziri wa maliasili na Utalii Costantine Kanyasu ameviagiza vyombo vya Dola kuendelea kulinda sehemu za mazalia ya samaki kwenye maziwa yote ya mkoa wa Rukwa ili kuruhusu samaki kuzalina kwa wingi kutokana na kukithiri kwa vitendo vya uvuvi haramu.
Alisema serikali haitaruhusu wananchi kuvua samaki kwenye sehemu zilizotengwa kama hifadhi kwani kwa kufanya hivyo kutasabisha samaki kupotea.
‘’hivyo ukirusu ziwa zima watu wavue, baada ya mda ziwa nzima tutakuwa hatuna samaki tena,hivyo kwa mukitadha huo ni lazima tukubaline kulinda maeneo yote yalitengwa na serikali kama hifadhi.’’alisema Kanyasu.
Aliyasema hayo kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika vijiji vya Ilanga na Kilingawana katika bonde la ziwa Rukwa wilaya ya Sumbanga mkoani Rukwa na kuwasihi wananachi kushirikina na maafisa nyama pori katika kulinda na kuhifadhi mazingira ya maziwa yalipo kwenye maeneo yao husika.
Kwaupande kaimu meneja wa pori la akiba la uwanda Thomas Njau aliwasihi wananchi kuacha kuvua samaki kwa kutumia zana haramu ikiwa ni pamoja na kuto vua samaki kwenye maeneo yaliotengwa na serikali kama hifadhi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.