Kituo cha ulinzi wa Rasilimali za uvuvi Kasanga wilayani Kalambo mkoani Rukwa kimefanikiwa kukamata nyavu haramu 127 kupitia msako mkali uliofanyika katika ziwa Tanganyika kupitia maeneo ya kata za Samazi na Kasanga.
Afisa Mfawidhi wa ulinzi wa Rasilimali za uvuvi kituo cha Kasanga Gasper Lugelelo, amesema zoezi hilo ni endelevu na kwamba kati ya nyavu hizo wamekamata vyandarua 15 ambavyo vilikuwa vikitumiwa na wavuvi kuvua dagaa kwenye ziwa hilo.
Baadhi ya wavuvi kutoka kata ya Kasanga na Samazi wilayani humo wameishauri serikali kuvifungia viwanda vyote vinavyozalisha nyavu haramu sambamba na kushirikiana na wavuvi katika kuwabaini na kuwakamata wasambazaji wa nyavu hizo ili kulinda mazalia ya samaki.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.