Uongozi wa Halmashauri ya Kalambo kupitia idara ya uvuvi imewaonya vikali wazazi na walezi wanao watumia watoto wadogo kuvua samaki kwenye ziwa Tanganyika na kusema kitendo hicho ni kinyume cha sheria.
Hatua hiyo inakuja baada ya wazazi na walezi katika vijiji vilivyopo Mwambao wa ziwa Tanganyika wilayani humo kuwatumia watoto wao katika shughuli za uvuvi na kusababisha baadhi yao kushindwa kuendelea na masomo na kujikita katika shughuli za uvuvi.
Afisa uvuvi wilayani humo Abduli Balozi,amesema kwa kutambua hilo wameanzisha ukaguzi kwenye vijiji vya Kipwa, Kapele ,Kasanga na Samazi kwa kukagua vyombo vyote vya uvuvi kisha kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani wazazi na walezi wenye tabia hiyo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.