...Mambo mbalimbali yamejadiliwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani cha robo ya Kwanza Mwaka wa fedha 2017/2018 ambao kilifunguliwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mh. Daud Sichone saa 4:00 asubuhi tarehe 21 Oktoba, 2017 na kumalizika Saa 7:30 Mchana. Katika Mkutano huo Wenyeviti wa kamati za kudumu waliwasilisha mihtasari ya Kamati zao na kutoa mwanya kwa wajumbe wa Mkutano huo kuhoji na kushauri mambo mbalimbali. Kamati hizo ni Kamati ya UKIMWI, Kamati ya Elimu, Afya na Maji, Kamati ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira pamoja na Kamati ya Fedha. Mkutano huo kinajumuhisha Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ambaye ni Katibu, Madiwani, Wakuu waIdarana Vitengo pamoja na wageni waalikwa pamoja na Waandishi wa Habari.
Mambo yaliyojitokeza katika kila Kamati:
Kamati ya UKIMWI (CMAC)
Ushauri: Idara ya Afya iwasihi watu naoenda kupima UKIMWI virus waache kwenda kupima sehemu nyingine mara baada ya kupatika na maambukizi pale wapopimwa sehemu moja, maana kwa kufanya hivyo inapelekea Wilaya kuonekana inatakwimu kubwa ya wenye maambukizi kitu ambacho si kweli.
Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
Ujenzi
Swali: Ni vipi Halmashauri imejipanga kutumia Mapato ya ndani katika ujenzi wa Majengo ya Shule na Zahanati yaliyoanzishwa kwa nguzu za Wananchi.
Ufafanuzi: Mkurugenzi Mtendaji, Ingawa kuna changamoto katika kiwango cha Mapato, Halmashauri imekuwa ikijitahidi kutenga fedha za ndani kwa ajili ya miradi za maendeleo katika uboreshaji wa majengo mbalimbali ya shule na zahanati ili kuhakikisha huduma inatolewa kwa Wananchi.
Swali: Ni kwa namna gani miradi iliyokuwa inasimamiwa na Halmashauri kupitia Idara ya Ujenzi itaendelezwa hasa ukizingatia watumishi wa Idara hiyo wamepelekwa kuunda Mamlaka inayojitegemea, Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA)
Ufafanuzi: Mkurugenzi mtendaji Mhandisi. Simon Ngagani amelieleza baraza kuwa ili kukamilisha miradi hiyo ataendelea kufanya mawasiliano na Meneja wa Mamraka ya Barabara Vijijini(TARURA) juu ya kuomba msaada wa Mamlaka yake kusaidia umaliziaji wa Miradi hiyo. Aidha amezisisitiza Serikali za Vijiji na Kata kuwaidhinisha mafundi wenye uwezo mzuri katika maeneo yao ili waweze kuwatumia katika ujenzi na ukarabati wa majengo ya Serikali zikiwemo shule na pamoja na vituo vituo vy afya/ zahanati.
Mkurugenzi Mtendaji akitoa ufafanuzi juu ya suala la umaliziaji wa Miradi iliyoanzishwa.
Uchumi
Swali: Halmashauri imejipanga vipi kuhakikisha wakulima wanapata tija katika msimu ujao wa Kilimo?
Ufafanuzi: Wakulima watapata tija katika kilimo kwa kuwa serikali imeshusha bei ya pembejeo za kilimo kama mbolea ambapo kwa sasa bei elekezi ya mbolea ni Tsh. 44,443 kwa mfuko ya UREA na Tsh. 57,022 Kwa mfuko wa DAP. Aidha amewataka Waheshimiwa Madiwani kuhimiza Wakulima juu ya kujiunga na vyama vya Ushirika ili kuweza kupata nafuu mbalimbali ikiwemo ya kukopeshwa mbolea.
Kamati ya Elimu Afya na Maji
Afya
Swali: Halmashauri inafanya nini kuhusu kutatua tatizo la vitanda katika vituo vyetu vya huduma ya afya kwa kuwa wagonjwa wamekua wakija na mikeka kama mbadala.
Ufafanuzi: Halmashauri imepokea vitanda 20, vikiwemo 3 vya kuzalishia kutoka Ofisi ya Rais ambavyo vimepelekwa katika vituo 17 katika Wilaya. Pia Halmashauri imepokea vitanda 17 vya kuzalishia kutoka Mamraka ya Bandari ambavyo vitasambazwa baada ya mapokezi rasmi.
Kaimu Mganga Mkuu Wilaya ya Kalambo Dr. Tusekile Kasanga akitokea ufafanuzi suala la uhaba wa vitanda katika Vituo vya Afya
Elimu
Swali: Halmashauri inajukumu gani kuongeza shule za Sekondari kidato cha tano na sita katika Halmashauri
Ufafanuzi: Halmashauri kupitia Idara ya Elimu Sekondari iliomba shule tatu kupewa hadhi ya kutoa elimu ya kidato cha tano na sita ambapo shule moja ya Mwazye imepewa hadhi hiyo. Aidha Mkuu wa elimu Sekondari amebainisha kuwa uhaba wa mihundombinu, bajeti ni sehemu ya changamoto ya uanzishaji wa shule za kidato cha tano na sita. Pia Afisa Elimu amewataka wananchi kijitolea katika ukarabati wa majengo ya shule zao .
Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya kalambo Bw. Ephraim Moses akitoa ufafanuzi juu ya uanzishaji shule mpya za Kidato cha tano na sita.
Maji
Swali:Ni kwa nini Mradi wa Maji Msanzi haujakamilika
Ufafanuzi: Mkurugenzi mtendaji ameanza kufuatilia utekelezaji wa Mradi huo katika kamati za Kata juu ya kusuasua kwa Mradi huu hvyo taarifa itatolewa baadae.
Swali: Kwa nini Mji wa Matai usifungwe mita katika mabomba ili kudhibiti matumizi mabaya ya Maji
Ufafanuzi: Mabomba yaliwekwa Mita ila kutokana na uchakavu mita hizo hazifanyi kazi, pia Mradi wa Maji Matai umefanyiwa tathimini upya ili kuendana na hadhi ya Makao Makuu ya Wilaya ambapo pindi utakapotekelezwa mita zitafungwa. Aidha anewataka Waheshimiwa Madiwani kuhimiza Wananchi katika maeneo yao juu ya uchangiaji wa huduma ya maji iki iwezekuwa endelevu.
Mhandisi wa Maji Wilaya ya Kalambo, Mhandisi Erast Vincent akitoa ufafanuzi juu ya suala la Maji.
Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
Akijibu swali la Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Daud Sichone linalohusu ni lini fedha za P4R (Malipo kwa Matokeo) zitapelekwa katika shule, MKurugenzi Mtendaji amejibu kuwa fedha hizo ziko tayari na zitapelekwa mashuleni hivi karibuni.
Kufunga Mkutano
Katibu wa Mkutano: Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi. Simon Ngagani amewataka Waheshimiwa Madiwani kuzikumbusha Serikali zao za Kata na Vijiji kuwa suala la Utawala bora ni suala linaloanzia ngazi ya chini, ngazi ya Kitongoji, hivyo ni vyema wakazingatia suala hilo ili kuondoa changamoto na migogoro isiyo ya lazima.
Mwenyekiti wa Halmashauri, Mh. Daudi Sichone aliwataka Waheshimiwa Madiwani kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza na kusimamia ukusanyaji wa mapato katika Maeneo yao ili kuongeza kiwango cha mapato katika Halmashauri. Aidha baada ya maneno hayo Mwenyekiti alifunga Mkutano huo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.