ZAIDI ya nyumba138 zimebomoka na watu139 kukosa makazi katika kijiji cha Kipwa kilichopo katika kata ya Kasanga wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa baada ya maji ya ziwa Tanganyika kuzingira makazi yao huku wahanga wa tukio hilo wakihifadhiwa kwa ndugu jamaa na majirani kutokana na nyumba zao kubomoka na nyingine kujaa maji.
Kijiji cha kipwa kinapatikana mpakani mwa nchi ya Tanzania na Zambia na kinajumla ya kaya 321, licha ya hilo kijiji hicho kilianza kuzingirwa na maji tangu february 2020 huku zaidi ya nyumba 138 zikibomoka mpaka kufikia hivi sasa.
Wakazi wa kijiji hicho wakiongozwa na Joseph Simtowe, wamebainisha kuwa hali ya maji kujaa katika maeneo hayo ilianza tangu februal 2020, ambapo maji yalianza kusogea taratibu na kujikuta kwenye wakati mgumu baada ya kusogea hadi kijijini na kuzingira makazi yao na baadhi yao kukosa mahali kwa kujihifadhi.
Walisema serikali hainabudi kuwasaidia vitu mbalimbali ikiwemo chakula, pamoja na matenti kwa lengo la kuwasaidia pindi watakapo hamia katika maeneo ya milima Mawesande ambako wanatarajia kuhamia hivi karibuni.
Hali hiyo imepelekea kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo Julieth Binyura , “tumeona madhara ni makubwa sana na tumechukua tathimini kwa kila nyumba ili siku tutakapo rudi tena tujue tunawasaidiaje” alisema Binyura.
Katibu tawala wilayani humo Frank Schalwe, alisema nyumba 139 zimeanguka na nyumaba 41 ziko hatarini kuanguka na kusema serikali itaendelea kuwa karibu ili kuweza kuwasaidia.
Afisa ardhi wilayani humo Nikoraus Ntajiri, alisema uongozi wa Halmashauri hiyo tayari umetenga maeneo mapya ya makazi katika milima wa Mawe sande na elimu imetolewa kwa wananchi juu ya kujenga kwa mipango miji.
Taarifa kutoka kijijini hapo zinaeleza kuwa tukio hilo ni la pili kujitokeza ambapo mwaka 2003 kijiji hicho kiliwahi kupata janga la moto na hivi sasa kujitokeza kwa maji ya ziwa hilo kuzingira makazi yao.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.