Mkuu wa wilaya ya kalambo mkoani Rukwa Julieth Binyura amezitaka kaya masikini zinazowezeshwa kupitia mfuko wa tasafu kuzitumia vizuri fedha wanazopatiwa na serikali kwa kuzielekeza zaidi katika shughuli mbalimbali za maendeleo yao binafusi na kuwasaidia kujikwamua na hali ya kiuchumi.
Binyura ameyasema hayo wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayofanywa wananufaika wa mpango wa tasafu katika vijiji vya Jengeni na Safu vilivyopo mpakani mwa nchi ya Tanzania na Zambia wilayani kalambo mkoani hapa.
Amesema amelazimika kuanzisha oparesheni ya ukaguzi wa wanufaika wa mradi huo kutokana na kuwepo kwa malalamiko kwa badhi ya maeneo kupewa fedha watu ambao sio walengwa wa mradi huo.
Mratibu wa mradi tasafu wilayani humo Michael Mwasumbi amesema fedha hizo hutolewa kulingana na hali
‘’kwa mwaka 2019 kaya 4545 katika vijiji 66 vimeingizwa kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini , ambapo kiasi cha shilingi milioni 1,244,000/=zimelipwa katika kijiji cha Jengeni na kiasi cha shilingi milioni 1,920,000/= zimelipwa katika kijiji cha Safu vyote vinapatikana mpakani mwa nchi ya Tanzania na Zambia.’’alisema Mwasumbi.
Baadhi ya wanufaika wa mfuko huo wilayani humo wamempongeza Raisi wa jamhuri ya mungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa kuwapatia fedha hizo kwani zimewasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuendeleza maisha yao.
Palizoni Mpinya mnufaika wa mpango wa tasafu katika kijiji cha Jengeni amesema wanampongeza Raisi Magufuli kwa kutoa fedha hizo kwani zimekuwa msaada mkubwa katika maisha yao kwa ujumla hususani katika kusimesha watoto waao pamoja na kuendeleza miradi mingine.
‘’tunasomesha watoto pia tunavaa kutokana na miradi ya tasafu, hivyo hatunasababu ya kumshukuru mh.Raisi kwa kutangalia sisi wanyonge hususani katika kutupatia fedha hizi.’’alisema mnufaika huyo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.