ZAIDI ya wakazi 35,954 kutoka vijiji kumi na sita (16) vya kata ya Mpombwe na Mkoe wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameanza kunufaika na uwepo wa vivutio vya utalii ikiwemo maporomko ya Kalambo fallse kutokana na serikali kupasua barabara mpya yenye urefu wa km16.0 kupitia hifadhi ya mto Kalambo ili kuwawezesha watalii kufika kwa urahisi ikiwa ni pamoja na wananchi kujiajili
Barabara hiyo yenye urefu wa km 16.0 imegharimu kiasi cha shilingi million 132. 7 na kupitia katika hifadhi asilia ya mto Kalambo kuelekea maporomoko ya Kalambo fallse yaliyopo mpakani kati ya nchi ya Tanzania na Zambia.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Kaimu Meneja wa wakala wa huduma za barabara za vijijini na mjini TARULA mkoani Rukwa, Rashid Katema, amebainisha kuwa mradi wa barabara ya Kawala Kapozwa ulisainiwa 20 may 2020 kati ya meneja wa kanda wakala wa huduma za misitu Tanzania kanda ya nyanda za juu kusini na mkandarasi M/s F.M.W Tradingi company limted.
Alisema mradi huo ulisainiwa kwa gharama ya shilingi million mia moja (100,000,000) na muda wa utekelezaji ikiwa ni mwezi mmoja.
“baada ya kusainiwa mkataba, mradi wa ujenzi wa barabara kilometa sita na mita mia sita kwa kiwango cha changarawe katika barabara ya Kawala –Kapozwa ulianza kutekelezwa kufukia mashimo madogo madogo yaliyokuwepo barabarani, kuchonga barabara kwa mkato mzito kilometa 6.6 (Heavy grading) kumwaga changarawe kilometa 4 pamoja na ulazaji wa makalavati.
Alisema mpaka sasa hajaomba fedha na amefanikiwa kufanya kazi kwa asilimia 90 na kusema kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya ufinyu wa bajeti ili kuikarabati barabra hiyo kila mwaka.
Meneja wa huduma za uhifadhi wa misitu Tanzania wilayani Kalambo Joseph Chezue, amesema msitu wa hifadhi ya Kalambo unaukubwa wa hekta 43,334 na mpaka wenye urefu wa kilometa 197 .71 na kusema msitu huo umerasimishwa kuwa mazingira asilia tangu februal 2019 kwa kuunganishwa misitu miwili yaani msitu wa hifadhi ya mto Kalambo na msitu wa Maporomoko ya Kalambo kuwa msitu wa hifadhi ya mazingira asilia.
Akikagua barabra hiyo mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo, amesema barabara hiyo inapaswa kukarabatiwa kila wakati ili iweze kupitika katika misimu yote kutokana na kuwa muhimu kwa utalii.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.