Zaidi ya watumishi 400 kutoka Halmashauri za Kalambo, Nkasi na Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa wameungana kwa pamoja na kuanzisha klabu ya mazoezi ya viungo vya mwili [AEROBICS EXERCISE] lengo likiwa ni kuimarisha afya zao ili kuepukana na magonjwa yatokanayo na uvivu,saikolojia na yasiyokuwa ya kuambukiza.
Akifungua klabu ya mazoezi hayo yaliyofanyika katika Wilaya ya Nkasi mkoani humo mganga mkuu wa mkoa Boniface Kasururu , amesema michezo ni afya na ni kinga ya maradhi mengi hivyo kila mwananchi anapaswa kuzingatia kauli iliyoungwa mkono na mkuu wa Wilaya ya Nkasi Saidi Mtanda.
Amesema kila mtu ana wajibu wa kushiriki kwenye mazoezi hayo kwani ni muhimu kwa afya zetu.
‘’sasa magonjwa ya kuambukiza yameshika kasi kubwa, kama vile kisukari na shinikizo la damu. Lakini kikubwa tunashauriwa kufanya mazoezi kila wakati ili kuondokana na matatizo kama hayo.’’
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Saidi Mtanda , aliwataka wananchi kujenga tabia ya kufanya mazoezi kila wakati kwa lengo la kusaidia mwili kuwa sawa, kuwaleta vijana pamoja ili waweze kubadilishana mawazo kwa ajili ya maendeleo yao ikiwa ni pamoja na kuepukana na magonjwa yasiyo kuwa ya kuambukiza.
Baadhi ya washiriki wa michezo hiyo ,wamesema licha ya kutekeleza agiz la Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hasan, michezo hiyo inawasaidia kuimarisha afya zao.
Afisa Utumishi na Utawala Wilayani Kalambo mkoani humo Amandus Mtani, amesema lengo la michezo hiyo ni kutekeleza agizo la makamu wa Rais ambalo alilitoa kwa kuwataka wananchi kufanya mazoezi.
‘’ Tunafanya mazoezi kwa sababu ni tiba na sio adhabu lakini kitu kinachotusumbua ni uvivu na uelewa mdogo.‘’Alisema Mtani.
Katibu wa michezo wilayani humo Baraka mazengo , alisema mwitikio wa watu ni mkubwa na kusema lengo kubwa ni kuhamasisha watu kushiriki kwenye michezo .
‘’tumekutana na makundi yote ya watu ambao wamefika eneo hilo na kushiriki kwenye michezo hii ya ambayo imefanyika hapa wilayani Nkasi.
Hata hivyo tangu kuanzishwa kwa mazoezi hayo, wilaya ya kalambo imefanikiwa kuwa na washiriki wapatao hamsini na kushiriki mazoezi hayo kila siku na kufanyika katika soko kuu la mazao Matai.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.