Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Pastory Mnyeti ametangaza mpango wa Serikali wa kupumzisha shughuli za uvuvi katika ziwa Tanganyika kwa miezi mitatu ili kuwezesha samaki kuzaliana na kuongeza tija kwa wavuvi wanaofanya shughuli za uvuvi Kwenye ziwa hilo.
Ametoa kauli ya serikali wakati akizungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Soko la samaki Kasanga Wilayani Kalambo mkoani Rukwa.
Alisema utekelezaji wa mpango huo utaanza rasmi Mei 15 hadi Agosti 15 mwaka huu ikiwa ni Utekelezaji wa Mkataba wa Kikanda wa Nchi Wanachama wa Mamlaka ya Ziwa Tanganyika unaoweka hatua na taratibu za usimamizi endelevu wa shughuli za uvuvi katika ziwa hilo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.