Mkuu wa wilaya ya Kalambo Dkt Lazaro Komba amewataka wananchi wilayani humo kuendelea kuwaenzi waasisi wa taifa la Tanzania kwa kufanya kazi kwa bidii kama sehemu kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanzania bara.
Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru wa Tanzania bara ambayo yamefanyika kwa kufanya usafi kuzunguka maeneo ya stendi ya mabasi wilayani humo na kuwataka wananchi wilayani humo kuenzi na kudumisha kazi nzuri zilizofanywa na waasisi wa taifa la Tanzania.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kalambo Shafi Mpenda ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi wilayani humo kulifanya zoezi la usafi wa mazingira kuwa endelevu ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.