Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Lazaro Komba amesema Halmashauri ya wilaya hiyo imejiwekea mkakati wa unyweshaji dawa za kinga tiba ya ugonjwa wa vikope(TRAKOMA) ili kufikia kiwango cha chini ya asilimia 5 kutokana na mambukizi ya ugonjwa huo kupungua kutoka asiliami 6 hadi kufikia asilimia 5 ya maambukizi.
Ameyabainisha hayo wakati wa uzinduzi wa zoezi la unyweshaji dawa za kingatiba ya ugonjwa wa vipoke ngazi ya jamii iliyofanyika katika eneo la Santamaria na kuwakilishwa na mtendaji kata ya Lyowa Sijali Msokele,mbapo amesema tafiti zinaonesha Halmashauri ya Kalambo kuwa na mambukizi ya ugonjwa wa Vikope kwa kiwango cha asilimia 6.
‘’ugonjwa wa vikope unashambulia macho, ambapo usipotibiwa mapema huweza kupelekea mgonjwa kupata upofu usioweza kutibika na kwamba ugonjwa huo husabababishwa na Bakteria aina ya Klamidia Trakomatis na kuenezwa na inzi kutoka kwa mgonjwa mwenye maambukizi kwenda kwa mgonjwa asiyekuwa na maambukizi’’ alisema Komba.
Kwa upande wake mratibu wa chanjo wilayani humo Zawadi Mwasomola alisema trakoma inapunguza uwezo wa kuona na kusababisha upofu na kwamba dalili zake ni pamoja na macho kuwasha,kuwa mekundu na maumivu makali kwenye macho ikiwa ni pamoja na kushindwa kuhimili mwanga na kuwataka wananchi kufika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya mara waonapo dalili hizo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.