Kaimu mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Kalambo Wambura Sunday amesema serikali haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani wazazi na walezi ambao watashindwa kuwaandikisha na kuwapeleka shule watoto wao ifikapo Januari 2025.
Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambayo kwa ngazi ya wilaya yamefanyika katika kata ya Katete wilayani humo na kusisitiza wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka shule watoto wao ifikapo Januari 2025 ikiwemo kuwaandalia mahitaji yao muhimu ya shule.
Kwa upande wake afisa ustawi wa jamii wilayani humo Hussein Kharimu ametumia fursa hiyo kuwataka wazazi na walezi kuwa sehemu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo kutoa taarifa za mtu au watu wanaojihusisha na vitendo vya ukatili.
Aidha amewataka wazazi na walezi kujenga mazoea ya kuwa karibu na watoto wao kwa ajili ya kujua changamoto zinazowakabili pindi wanaporudi kutoka shule na kusisitiza viongozi wa serikali za vijiji kuwa sehemu ya kusuluhisha migogoro ya kifamilia ili kuwawezesha watoto kulelewa katika mazingira bora na wezeshi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.