Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Wilayani Kalambo mkoani Rukwa imeanzisha mkakati maalumu utakao wawezesha wananchi kufanya utalii wa ndani kila jumamosi ya kila mwezi kwa kutembelea maanguko ya maji ya mto Kalambo na hifadhi asilia ya mazingira Kalambo ili kuwawezesha wananchi kujifunza na kujionea aina mbalimbali za wanyama na mimea.
Hayo yamebainishwa na meneja wa wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Wilayani Kalambo ndugu Brayson Mkiwa wakati akiongea na watalii wa ndani ambao walikuwa wametembelea maanguko ya maji ya mto Kalambo na kusema uwepo wa utalii huo utasaidia jamii Kujifunza umuhimu wa utunzaji mazingira.
Aidha amesema licha ya hilo, pia wamefanikiwa kuadhimisha siku ya wapendanao (VALENTINE DAY) ambayo waliifanya kwa kutembelea hifadhi ya mazingira Kalambo sambamba na kupanda ngazi za maanguko ya maji ya mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa urefu barani afrika kwa mita 235 kutoka maji yanapoanzia.
Baadhi ya watalii wa ndani waliotembelea maanguko hayo akiwemo Francis Nkemwa ,wameipongeza serikali kupitia wakala wa huduma za misitu Tanzania Kwa kuboresha miundombinu ya ngazi na Barabara katika maeneo hayo ambayo yamekuwa yakiwezesha wananchi kufika kwa urahisi zaidi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.