Watumishi wa umma katika Halmashuri ya Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa wamewatakiwa kufanya kazi kwa bidii, weledi, nidhamu, uadilifu na ubunifu ili kutimiza malengo na maono ya serikali katika kuwaletea maendeleo Watanzania
Hayo yamebainishwa na mkuu wa idara ya utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wilayani humo Ndugu Amandus Mtani kupitia kikao cha kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za watumishi wa umma wilayani humo na kusema kila mtumishi anapaswa kutambua kuwa mafanikio katika utekelezaji wa majukumu,mipango na mikakati wanayoisimamia yanahitaji juhudi ya kila mtumishi na nidhamu katika kufanya kazi.
“Nitoe wito kwa kila mtumishi kuzingatia nidhamu ya kazi na maadili ya utumishi wa umma, kwani Serikali ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatekeleza falsafa ya Kazi Iendelee. Kwa msingi huo watumishi wote wa umma mnao wajibu wa kufuata na kutekeleza falsafa hii kwa vitendo kwani haki huletwa na wajibu.” Alisema Mtani
Aidha ametumia fursa hiyo kuwapongeza watumishi hao kwa kuendelea kutekeleza majukumu yao vizuri na kwa weledi. “Kujituma kwenu, ushirikiano na bidii vimewezesha Serikali na hususani Ofisi ya mkurugenzi mtendaji kupata mafanikio makubwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na ukusanyaji Mapato’’ Alisema Mtani.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.