Mkuu wa Idara ya utawala na usimamizi wa Rasilimali watu katika Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Amandus Mtani amewataka watumishi wa umma kujenga utamaduni wa kuwahi kazini ili kuwezesha wananchi kupata huduma bora na kwa wakati.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa umma katika jengo la utawala la halmashauri hiyo ikiwa ni utekelezaji wa kawaida wa kanuni za kudumu za utumishi wa umma na kusema
“Nasema hili,siyo kwamba watumishi wote mnachelewa, hapana. Lakini nalisisitiza kwa sababu wapo watumishi wachache wanaochelewa na kuchelewa kwao kunasababisha ucheleweshaji wa kutoa huduma” alisema Mtani.
Pamoja na mambo mengine amewataka watumishi kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia miongozo ya serikali ikiwa ni pamoja na kujiepusha na vitendo vya Rushwa.
“Mnajua nyie maafisa ni watawala katika maeneo yenu. Na sifa ya mtawala ni kutokuwa na viashiria vya rushwa.Mnatakiwa kusimamia haki katika utendaji wenu wa kazi ili wananchi wapate huduma bora” Alisisitiza Mtani.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.