Na IO - Kalambo
Baraza la madiwani wilayani Kalambo mkoani Rukwa limepitisha mapendekezo ya bajeti ya shilingi Billion 32.148 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kati ya hizo billion 17 ,697,59,000.00 ikiwa ni misharahara na shilingi billion 11,435,843,000.00 ikiwa ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo
Mapema akiwasilisha mapendekezo ya bajeti hiyo kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo afisa mipango na uratibu Erasto Mwasanja , alisema kati ya fedha hizo shilling 87,222.00 sawa na asilimia 2.60 ya bajeti nzima ni kwa ajili ya matumizi mengineyo na kwamba kwa mwaka wa fedha 2023/ 2024 Halmashauri imekadiria kukusanya fedha billion 2,180,150,000.00.kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya mapato.
Alisema miongoni mwa vyanzo ambavyo vitakusanywa ni pamoja na ushuru wa mazao ,ushuru wa huduma mbalimbali , ada za Lesen za biashara, ushuru wa mazao ya mifugo,adhabu mbalimbali , ushuru wa samaki na vyombo vya uvuvi ,Raslimali za Aridhi,mazao ya misitu , ujenzi, manunuzi,sheria na Tehama
Mapema akiongea kupitia kikao hicho mkuu wa wilaya ya Kalambo Lazaro Komba , aliwataka watumishi kubuni vyanzo vipya vya mapato ambayo vitasaidia katika kuibua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo vituo vya Afya na zahanati
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.