Wilaya kupitia sekta ya Maendeleo ya Jamii imefanikiwa kusajili vikundi vya kijamii 217. Kati ya vikundi hivyo, vikundi 11 vya wanawake na vijana vimeweza kupatiwa mkopo wenye jumla ya shilingi 17,144,000/= kupitia mfuko wa WDF na kikundi kimoja cha vijana kati ya hivyo kimepatiwa mkopo kutoka Wizara ya Vijana, Utamaduni na Michezo. Kati ya Vikundi hivyo 11, vikundi vine (4) vimerejesha mkopo wote mapema na vilivyobaki saba (7) bado havijarejesha mkopo wao wa kiasi cha Tshs.10,326,000/=.
Mpango wa kunusuru kaya maskini – TASAF
Wilaya ya Kalambo kupitia Mfuko wa TASAF awamu ya tatu katika kipindi cha Julai 2015 hadi Juni 2016 imepokea Jumla ya shilingi 1,198,188,000/=, ambapo matumizi yake ni kiasi cha shilingi 1,197,079,757.28 kupitia Mpango wa kunusuru kaya masikini. Kaya zipatazo 4,674 zimeweza kufikiwa kupitia mpango huu katika vijiji 66 vilivyopo kwenye mpango.
Taarifa dhidi ya mapambano ya UKIMWI
Wilaya ina wateja 1195 wa tiba na matunzo, na walio katika dawa za kupunguza makali ya VVU/UKIMWI ni 1098, na watoto chini ya miaka 5 walioko katika dawa ni 57.
Huduma zitolewazo na Sekta ya Ukimwi
Mafanikio dhidi ya maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.