Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Dkt, Lazaro Komba amekabidhi pikipiki 3 kwa maafisa mifugo zitakazo Saidia kufanya ufuatiliaji wa magonjwa ya mifugo na utoaji wa chanjo na kuwataka maafisa mifugo kuweka mfumo rafiki utakao wezesha upatikanaji wa mbegu bora za mifugo ambazo zitawezesha wafugaji kuzalisha na kufuga kwa tija.
Ameyasema hayo wakati akikabidhi pikipiki 3 kwa maafisa mifugo wilayani humo na kusema lengo la serikali ni kurahisha shughuli za utendaji kazi ikiwemo ufuatiliaji wa magonjwa ya mifugo na utoaji chanjo kwenye mifugo.
Pamoja na mambo mengine amewataka kuzingatia utunzaji wa vifaa hivyo ili viweze kudumu kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Edifonce Kanoni ametumia fursa hiyo kuipongeza Serikali kwa kutoa vitendea kazi hivyo na kuwataka wafugaji kufuga kisasa na kwa tija ikiwemo kutafuta mbegu bora za mifugo ambazo zitawawezesha kupata mavuno bora.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ambae pia ni Mkuu wa Divishen ya kilimo na mifugo Ndugu Nicholaus Mlango ametumia fursa hiyo kuwataka maafisa hao kufanya kazi kwa weledi na kwakuzingatia miongozo ya Serikali.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.