Kinasimamia shughuli zote zihusuzo manunuzi katika Taasisi nunuzi
Kinasaidia kazi za Bodi ya Zabuni
Kinatekeleza kazi za Bodi ya Zabuni
Ni sekretarieti kwa Bodi ya Zabuni
Kinapanga na kuratibu kazi zote za manunuzi za Taasisi Nunuzi
Inashauri Taasisi nunuzi njia gani ya kufanya manunuzi kulingana na thamani ya manunuzi yanayotakiwa kufanyika
Inaangalia na kuandaa mahitaji ya Kitalaam ikishirikiana na Idara Tumizi
Kinaandaa makablasha ya zabuni
Kinaandaa matangazo kwaajili ya fursa mbalimbali za kimanunuzi katika Taasisi nunuzi
Kinaandaa makabrasha ya mikataba mbalimbali
Kinagawa makabrasha mbalimbali yaliyoidhinishwa na Bodi ya Zabuni kwa wakandarasi /watoa Huduma na Wazabuni mbalimbali pale fursa ya kimanunuzi inapotekea
Kinatunza nyaraka na michakato yote ya kimanunuzi
Inatunza orodha yote ya mikataba iliyoingia na Taasisi nunuzi
Inaandaa Taarifa za kila mwezi za manunuzi na kuziwasilisha Bodi ya Zabuni
Kinaandaa na kuwasilisha kwenye kikao cha watalaam wa Halmashauri taarifa ya manunuzi ya kila robo ya mwaka inayotekelezwa kwa kufuata mpango wa manunuzi (Procurement Plan)
Inaratibu na kusimamia shughuli zote za kimanunuzi kwa Idara zote na Vitengo vyote katika Taasisi nunuzi
Kinaandaa taarifa nyingine ikiwa kama zitahitajika wakati wowote kwa Bodi ya Zabuni,Afisa masuuli au mamlaka nyingine zilizopo kwa mujibu wa sheria
IDARA TUMIZI (USER DEPARTMENT)
KAZI ZA IDARA TUMIZI
Inaanzilisha mchakato wa manunuzi ya idara au kitengo chake na kuwasilisha kitengo cha Manunuzi
Inaandaa mahitaji ya kitalaam katika mahitaji ya msingi ya Idara pamoja na Hadidu za rejea kwa Kitengo cha Manunuzi
Kinapendekeza maelezo ya mahitaji ,viwango na vipimo kwa kitengo cha Manunuzi
Kinashiriki kufanya Tathmini ya kazi mbalimbali kwa kupitia mwakilishi wa Idara au Kitengo kwa kuungana na Timu iliyopendekezwa kufanya kazi hiyo na Mkurugenzi Mtendaji
Inatoa taarifa yoyote ihusuyo kutokukidhi kwa vigezo na masharti kwa mkataba uliosainiwa kkwa kitengo cha Manunuzi .
Inapeleke taarifa zozote za mabadiliko ya mkataba kwenye kitengo cha Manunuzi kwa ajili ya kuwasilisha kitengo cha manunuzi ,bodi ya Zabuni au kwa Afisa Masuuli
Inaangalia utekelezaji wa mikataba yote inayosimamiwa na Idara yao ikiwemo kupitia na kuridhia mahitaji ya kiufundi au jambo lolote la ki -mkataba wakishirikiana na Kitengo cha Manunuzi wakati wa uandaaji wa Bajeti.
BODI YA ZABUNI
KAZI ZA BODI YA ZABUNI
Inafanyia kazi mapendekezo toka kwa Kitengo cha Manunuzi na kuridhia usainishwaji wa mikataba mbalimbali ya kazi
Inapitia maombi yote ya ongezeko la muda , kazi au usitishaji wa mikataba yoyote inayoendelea kutekelezwa ikwa ina kasoro ya utekelezwaji wake
Inaridhia njia inayotumika katika kufanya manunuzi ya umma
Inahakikisha kuwa Taasisi nunuzi inazingatia sheria na kanuni za ununuzi wa umma