Wilaya kupitia Sekta ya Ardhi imeendelea na majukumu yake ya upimaji wa viwanja, upangaji miji, utatuzi wa migogoro ya Ardhi na umilikishaji wa Ardhi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria.
Hadi kufikia Agosti 2016, maeneo mbalimbali ya Wilaya yamepimwa ambapo jumla ya viwanja 1,538 vimepimwa kama inavyoonyesha kwenye jedwali hapo chini.
Jedwali Na. 24: Maeneo yaliyopimwa viwanja.
Eneo/Kata
|
Lyowa
|
Kasanga
|
Matai
|
Mikonko
|
Kapozwa
|
Mkangale
|
Idadi ya viwanja |
182 |
414 |
531 |
34 |
365 |
12 |
Chanzo: Idara ya Ardhi Agosti 2016
Jumla ya hati miliki 331 za kisheria na hati miliki za kimila 390 zimetolewa.
Mpango wa uandaaji wa ‘Master Plan’ ya miji yetu.
Kutokana na gharama kubwa za uandaaji wa master plan, mpaka sasa Wilaya haijaweza kuandaa ‘Master Plan’. Katika kukabiliana na changamoto hiyo Wilaya kupitia idara ya Ardhi imeandaa michoro ya mipango miji 16 yenye viwanja 6,170 vya matumizi mbalimbali na upimaji zaidi unaendelea ili kuzuia ujenzi holela.
Ulipaji wa fidia kwenye maeneo yaliyofanyiwa uthamini.
Wilaya kupitia idara ya ardhi imefanya uthamini kwa ajili ya fidia kwa wananchi 47 ambao maeneo yao yalitwaliwa kupisha uchimbaji wa mfereji wa kuzuia maji toka mlimani, ujenzi wa barabara na baadhi ya maeneo yaliyopimwa viwanja. Hadi kufikia tarehe 30, Julai 2016 wananchi 7 kati ya 47 wamelipwa kiasi cha shilingi 4,960,632 fedha zilizotokana na mauzo ya fomu za maombi ya viwanja. Pia tutaendelea kulipa fidia kwa wananchi wote kadiri tutakavyo pata fedha kutokana na mauzo ya viwanja.
Mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Kutokana na ufinyu wa Bajeti Wilaya imeweza kuandaa mpango wa matumizi bora ya Ardhi kwa Vijiji 12 kati ya vijiji 111 vilivyopo. Wilaya inatambua kuwa mpango wa matumizi bora ya ardhi ni njia pekee ya kuondoa migogoro mingi ya ardhi inayojitokeza baina ya wakulima na wafugaji. Wilaya itaendelea kupima na kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi wa vijiji vilivyobaki kadiri fedha itakavyokuwa inapatikana.
Migogoro ya ardhi na utatuzi wake.
Ulijitokeza mgogoro wa kijiji cha Katapulo na kampuni ya ranchi ya kalambo na ukatatuliwa na mkurugenzi wa upimaji ramani ambaye alitoa maelekezo kwa kijiji kuzingatia mipaka iliyopimwa. Pia mgogoro wa Serikali ya Kijiji cha Mao na Mwananchi mmoja, wataalam toka ngazi ya Wilaya walifanya usuluhishi lakini pande hizo mbili hazikukubaliana kwa ufumbuzi zaidi wataalam walimshauri Mwananchi anayelalamika apeleke
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.