Idara ya Maji ipo kwa mujibu wa muundo wa Utumishi ikiwa na jukumu kubwa la kutoa huduma ya maji kwa wakazi wa Wilaya ya Kalambo. Pamoja na jukumu la kutoa huduma ya maji Idara inahusika na kupanga na kusanifu miradi ya maji, kupitia usanifu wa miradi ya maji unaofanywa na wataalam wa nje, kusimamia ujenzi na uendeshaji wa miradi ya maji pamoja na kukarabati miradi ya maji yenye hitilafu. Idara pia inahusika na kuunda na kusimamia vyombo vya watumiaji maji
Malengo/Majukumu ya Idara ya Maji
1. Kuandaa bajeti ya kutekeleza miradi ya maji na kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo
2. Kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa Wilaya wasiopata huduma ya maji.
3. Kupunguza na kuzuia milipuko ya magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa maji safi na salama
4. Kusimamia vyema miradi inayofanya kazi kwa kusisitiza vyombo vya kusimamia
Wilaya ina visima vifupi 14 vinavyofanyakazi na 25 visivyofanyakazi, visima virefu 68 vinavyofanyakazi na 63 visivyofanya kazi, miradi ya bomba ya mtiririko 8 inayofanya kazi na 4 isiyofanyakazi, miradi miwili ya maji ya kusukuma kwa mashine chemichemi zilizohifadhiwa 10 na miundombinu ya kuvuna maji ya mvua katika taasisi mbalimbali. Aidha miradi yote tajwa hapo juu ina jumla ya vituo 463 ambapo vituo 316 vinafanyakazi vinakadiria kuhudumia wananchi wapatao 96,200.
Wilaya ya Kalambo inatekeleza Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji kwa mpango wa vijiji 10 na vijiji vya nyongeza yaani vya Quickwins.
Miradi iliyotekelezwa kupitia Miradi ya maendeleo ya maji ni.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.