Wilaya ya Kalambo ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za Afya 59, kati ya hivyo, vituo vya afya 4 na zahanati 55. Zahanati 5 kati ya 55 zinaendeshwa na mashirika ya dini (FBOs).
Magonjwa kumi (10) yanayoathiri zaidi wananchi
Katika Wilaya ya Kalambo magonjwa kumi (10) yanayoathiri zaidi wananchi ni malaria, magonjwa yanayoathiri mfumo wa upumuaji, kuhara, vichomi, magonjwa ya yanayoathiri mfumo wa mkojo (U.T.I), minyoo ya tumbo, pumu, magonjwa ya ngozi, magonjwa ya macho na magonjwa yanayohitaji upasuaji mdogo kama majipu.
Aidha wagonjwa wa nje kwa mwaka wa fedha 2015/2016 wamepungua kwa asilimia 14.5 ukilinganisha na mwaka 2014/2015 pia wagonjwa wa ndani wamepungua kwa asilimia 30.4
Jedwali Na. 16: Idadi wagojwa wa nje na ndani
Wagonjwa |
Mwaka |
Tofauti |
% Tofauti |
|
2014/2015
|
2015/2016
|
|||
Wagonjwa wa nje
|
108,788 |
95,014 |
13,774 |
14.5 |
Wagonjwa wa ndani
|
1,411 |
1,082 |
329 |
30.4 |
Chanzo: Ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya, Julai, 2016.
Huduma za chanjo ya mama na mtoto
Wilaya ya Kalambo inaendelea na zoezi la utoaji chanjo ya mama na mtoto na kutoa elimu kwa Jamii juu ya chanjo hizo kupitia Sekta ya Afya. Kwa kipindi cha Januari mpaka Disemba, 2015 wastani wa watoto 11,000 walipatiwa chanjo (sawa na Asilimia 99.4) kati ya watoto 11,069, pia kati ya akina mama 11,069 waliopatiwa chanjo ya pepopunda (T.T 2+) ni 8,264 (sawa na asilimia 74.6).
Halikadhalika kwa kipindi cha Januari mpaka Mei, 2016 wastani wa watoto 5,349 walipatiwa chanjo (sawa na Asilimia 52.0) kati ya watoto 10,348, pia kati ya akina mama 10,348 waliopatiwa chanjo (T.T 2+) ni 2,680 (sawa na asilimia 25.9).
Jedwali Na. 17: Chanjo zitolewazo na idadi ya walengwa
Na. |
Aina ya chanjo |
Januari hadi Disemba, 2015 |
Januari hadi May, 2016 |
||||
Idadi ya Walengwa
|
Idadi ya Waliopatiwa chanjo
|
%
|
Idadi ya Walengwa
|
Idadi ya Waliopatiwa chanjo
|
%
|
||
1 |
BCG
|
11,069 |
11,046 |
99.8 |
10,348 |
7,330 |
70.8 |
2 |
DPT – HB
|
11,069 |
11,046 |
99.8 |
10,348 |
4,836 |
46.7 |
3 |
0PV – 3
|
11,069 |
10,952 |
98.9 |
10,348 |
5,008 |
48.4 |
4 |
ROTA-2
|
11,069 |
10,886 |
98.3 |
10,348 |
4,935 |
47.7 |
5 |
MEASLES/Rubella
|
11,069 |
11,029 |
99.6 |
10,348 |
5,104 |
49.3 |
6 |
PCV -3
|
11,069 |
11,043 |
99.8 |
10,348 |
4,879 |
47.1 |
7 |
T.T -2+
|
11,069 |
8,262 |
74.6 |
10,348 |
2,680 |
25.9 |
Chanzo: Ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya, Julai 2016
Mafanikio katika utoaji wa huduma za afya.
Wilaya ya Kalambo kupitia Sekta ya Afya Katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2016 katika jitihada za kuboresha utoaji na upatikanaji wa huduma za Afya imefanikiwa katika maeneo yafuatayo:-
Halmashauri kwa kushirikiana na wadau imefanikiwa kujenga vyumba vitatu vya upasuaji katika vituo vya Afya Matai, Mwimbi na Ngorotwa.
Takwinu: Ofisi ya Mganga Mkuu Wilaya Julai 2016
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.