UTANGULIZI
Idara ya Mazingira na udhibiti wa taka ngumu ni miongoni mwa Idara zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo. Idara hii bado ina mtumishi mmoja tu ambaye ni Kaimu Mkuu wa Idara. Katika hali ya kawaida Idara hii inatakiwa kuwa na Maafisa Afya Mazingira, Maafisa Mazingira na Wahudumu wa usafi lakini kwa sasa Idara hii haina watumishi hao. Hata hivyo Idara hii imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na Maafisa Afya waliopo katika Idara ya Afya.
Majukumu ya Idara ya Mazingira na udhibiti wa taka ngumu ni haya yafuatayo:-
•Kusimamia usalama wa maji
•Kusimamia usalama wa vyakula
•Udhibiti taka ( Taka ngumu )
•Udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza
•Kusimamia ujenzi wa ubora wa nyumba
•Udhibiti wa uchafuzi wa hali ya hewa
•Usalama wa Afya kazini
•Usalama wa Afya bandarini, mipakani na viwanja vya ndege
•Utoaji wa elimu ya afya ya mazingira na usafi ( Health sanitation and Hygiene Education )
•Ukaguzi wa afya ya mazingira
•Kufanya utafiti wa kina mara kwa mara kubaini vyanzo vya uchafuzi wa mazingira na athari zake
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.