Hamashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imeanzisha mpango mkakati wa kupata waamuzi na makocha wa mchezo wa netboli kwa kuwajengea uwezo walimu wa michezo,maafisa michezo na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ili kujua sheria pamoja na mbinu mbalimbali za michezo.
Akiongea kupitia mafunzo hayo kaimu mkuu wa kitengo cha michezo utamaduni na sanaa wilayani humo Ndugu Amos Mmewa amebainisha kuwa lengo ni kuwawezesha walimu na wanafunzi kujua mabadiriko ya sheria mbalimbali za mchezo wa netboli.
Aidha ametumia fursa hiyo kuwataka washiriki wa mafunzo hayo kuyatumia mafunzo hayo katika shule na vitalu vya michezo kwa lengo la kukuza na kuendeleza mchezo wa netboli.
Hata hivyo baadhi ya walimu wa michezo wilayani humo ambao licha ya kuupongeza uongozi wa Halmashauari hiyo kwa kuanzisha mpango huo, wameomba mafunzo hayo kuwa endelevu kwani yatasadia kuendeleza na kukuza mchezo husika na hatimaye kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ikiwemo mashindano ya michezo ya UMITASHUMTA, UMISSETA na SHIMISEMITA.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.