Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imepokea Trekta ndogo za mkono (PowerTillers) 11 kutoka Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Umwagiliaji ili kuongeza na kuimarisha Upatikanaji wa huduma za zana za kilimo katika mnyororo wa uzalishaji wa mazao ya kilimo kulingana na mahitaji ya wadau hususani wakulima wadogo.
Akikabidhi zana hizo mkuu wa wilaya hiyo Dkt, Lazaro Komba amesema lengo la serikali ni kuwawezesha wakulima kuongeza uzalishaji mazao ya nafaka na kuwaagiza maafisa kilimo kuweka utaratibu mzuri utakaowezesha mitambo hiyo kufanyiwa ukarabati mara kwa mara ili kuifanya kudumu kwa muda mrefu.
Aidha amebainisha kuwa Wakulima watazalisha kwa wakati na kwa urahisi na kuwezesha kupatikana kwa ziada ya mazao ambapo watauza na kuongeza ushuru wa mazao utakaowezesha Halmashauri kukusanya mapato kwa wingi.
Mbunge wa jimbo hilo Mhe.Edfonce Kanoni ametumia fursa hiyo kuwataka wakulima kuzingatia kanuni bora za kilimo ikiwemo kushirikana na wataalam wa kilimo wakati wa kuandaaji mashamba.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Ndugu Nicholas Mrango amebainisha kuwa Halmashauri imeanisha maeoneo yatakayofaa kujenga vituo vya zana za kilimo ikiwemo kituo cha kata ya Matai, Lyowa na Msanzi ambapo taratibu za kuanzisha ujenzi wa vituo hivyo zinafanywa na Wizara ya kilimo.
‘’kwa sasa zana hizi za kilimo zitatunzwa katika maeneo yaliyoanishwa chini ya uongozi wa serikali ya kata na vijiji kwa kushirikiana na Maafisa Kilimo na Maoperator.’’ Alisema Mrango.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.