Mkuu wa wilaya ya kalambo mkoani Rukwa Lazaro Komba amewataka Wananchi wilayani humo kuzingatia matumizi sahihi ya uhifadhi mazao ya nafaka ikiwemo kutumia teknolojia mpya ya uhifadhi kwa mifuko ya kinga njaa ili kujiepusha na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo yanaweza kujitokeza kutokana na matumizi ya viatilifu.
Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mifuko ya kinga njaa (PICS) kupitia hafla iliyofanyika katika kijiji cha Msanzi wilayani humo, ambapo amesema mifuko hiyo ina uwezo wa kumudu kwa zaidi ya miaka 3 na hivyo kupunguza gharama za uhifadhi mazao ambazo zimekuwa zikijitokeza kutokana na kufanya manunuzi ya mifuko ya kawaida kila mwaka.
Amesema uhifadhi kwa kutumia njia ya mifuko ya kinga njaa (PICS) ni salama zaidi kuliko uhifadhi kwa njia ya mifuko ya kawaida na kusisitiza wananchi kutumia mfumo huo ili kulinda afya na mazao kutoharibiwa na wadudu waharibifu.
Kwa upande wake Adam Ngomela ambaye ni Mtaalamu mwelekezi wa matumizi Ya Mifuko Ya PCS,amesema katika msimu wa mwaka 2022/2023 chini ya usimamizi wa shirika la Briteni wamefanikiwa kuwatembelea na kuwafikia wakulima 4246 kwa kuwajengea uwezo kwa vitendo dhidi ya matumizi sahihi ya mifuko ya kinga jaa (PCS).
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.