Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imefanikiwa kuhesabu Kaya 65,846 sawa na asilimia 99.93 kati ya kaya 65 ,894 ambao walikisiwa kuhesabiwa tangu kuanza kwa zoezi la sensa na makazi Agosti 23/2022 huku wananchi waliopata fursa ya kuhesabiwa kwenye zoezi hilo wakiipongeza serikali kwa kuweka mazingira rafiki na wezeshi yaliyowezesha kuhesabiwa kwa haraka na kuendelea na shughuli zingine za ujenzi wa taifa.
Zoezi la sensa na makazi Lilianza kufanyika rasmi kitaifa Agosti 23/2022 ambapo kwa wilaya ya Kalambo zoezi hilo lilianzia katika makazi ya mkuu wa wilaya hiyo Tano Mwela ambaye mnamo majira ya saa sita usiku na dak 1 alihesabiwa kama raia namba moja wa wilaya hiyo na kufuatiwa na mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri hiyo Shafi Mpenda.
Hata hivyo tangu kuanza kwa zoezi hilo wananchi walionyesha mwitiko mkubwa kwa kujitokeza kuhesabiwa na kutoa ushirikiano kwa makarani wa zoezi hilo hatua iliyopelekea kumalizika haraka kwa zoezi hilo.
Awali akiongea baada ya kamati ya usalama ya wilaya hiyo kutembelea na kukagua maendeleo ya zoezi la sensa na makazi katika maeneo tofauti ya wilaya hiyo, Mkuu wa wilaya hiyo Tano Mwela , alisema zoezi hilo limekwenda vizuri na kufanikiwa kufikia malengo ya serikali.
‘’Wilaya yetu ya Kalambo tulikuwa na maoteo ya kuhesabu watu 65,894 na mpaka sasa tumefanikiwa kuhesabu kaya 65,846 sawa na asilimia 99.93 kwa hiyo tumefanikiwa kuhesabu watu wote kwa wilaya ya kalambo na kama kuna waliobakia basi ni wachache sana ambao tunaendelea kuwamalizia.’’Alisema Mwela.’’
Licha ya hilo alilisitiza wananchi kutoa ushirikiano wakati wa dodoso la majengo ambalo linatarajiwa kuanza kufanyika Rasmi Agosti 30/2022.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.