Maafisa maendeleo ya jamii katika halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa wamekabidhiwa pikipiki zitakazo Saidia kurahisisha mawasiliano na ufuatiliaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi vijijini.
Makabidhiano ya pikipiki hizo yamefanywa na Naibu katibu mkuu wizara ya maendeleo ya jamii, Jinsia,Wanawake na makundi maalumu,Bi.felister Mdem na kusema lengo la serikali ni kuongeza ufanisi wa kazi kwa maafisa maendeleo ya jamii hususani wakati wa utoaji elimu kwa wananchi.
Awali akikabidhiwa pikipiki hizo kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Kalambo Ndugu Sandy Wambura,amesema Halmashauri ya Kalambo imepata pikipiki mbili (2) kati ya pikipiki 8 zilizotolewa na serikali na kusema pikipiki hizo zitaongeza kasi ya utoaji huduma na kufikisha elimu ya maendeleo kwa wananchi kwa muda muafaka.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.