Daraja la Kale lililopo katika kata ya Ulumi linalounganisha vijiji 11 vya kata 3 za wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa limesombwa na maji kufuatia mvua kubwa ilionyesha katika maeneo hayo na kusababisha kukatika kwa mawasilino ya barabara.
Wananchi katika maeneo hayo wamesema daraja hilo linaunganisha vijiji 11 kutoka kata za Ulumi,Mambwekenya na Mnamba na kuelezea kuwa ili kuyafikia maeneo hayo ni lazima upitie na kuvuka kwenye daraja hilo na kuiomba serikali kuharakisha ujenzi wa daraja hilo.
Meneja wa TANROAD mkoani Rukwa Mhandis Mgeni Mwanga , alisema serikali imeanza jitihada za kuusafisha mto huo na kuweka mawe lengo likiwa ni kuweka kivuko cha muda wakati wakisubiri bajeti ya daraja kubwa kujengwa kwenye mto huo.
Aidha aliwasisitiza wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati serikali ikiendelea kufanya jitihada za makusudi za kujenga kivuko hicho.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.