Halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa imefanikiwa kusajiri vikundi 31 vya wanawake vijana na wenye ulemavu kwa mwaka 2020/2021 huku jumla ya fedha tasilim shilingi million sitini ( 60,000,000/=) zikikopeshwa kwenye vikundi hivyo kwa lengo la kuvijengea uwezo kiuchumi na kupunguza umasikini wa kipato.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na idara ya Maendeleo ya jamii hivi karibuni kupitia baraza la madiwani la robo ya nne ya mwaka 2020/2021 wilayani humo, ilielezwa kuwa kazi zingine zilizofanyika ni pamoja na uhamasishaji jamii kwenye ujenzi wa miradi ya maendeleo, kuratibu shughuli zinazofanywa na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali, kunusuru kaya masikini kupitia mpango wa TASAFU III unaotekelezwa katika vijiji 66 kupitia uhaulishaji fedha kwa kaya masikini 4,312 ambapo jumla ya shilingi million 927,168,460 zilitolewa hadi kufikiia juni 30/2021.
Hata hivyo, kupitia zoezi la hivi karibuni la utambuzi na uandikishaji wa kaya masikini katika vijiji 45 vilivyokuwa nje ya mpango huo, Halmashauri imepata mafanikio makubwa ambapo jumla ya kaya 5,270 zilidodoswa kwa wawezeshaji kutembea kaya kwa kaya kwa lengo la kuingiza taarifa muhimu zinazotakiwa kwenye mpango,
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.