Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amesisitiza umoja na mshikamano kwa waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)ambao kwa majuma kadhaa wamekuwa na mikwaruzano hali iliyofanya waumini hao kuswali kwa mafungu jambo ambalo halileti maendeleo ndani ya kanisa pamoja na mkoa.
Amesema kuwa wakati alipoteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kuweza kuwasili katika mkoa miongoni mwa viongozi wa dini waliomuombea alikuwa ni Baba Askofu Ambele Mwaipopo ambaye anatambuliwa na serikali na kutahadharisha kuwa endapo serikali inamtambua kuwa ndio kiongozi wa kanisa hilo iweje wanaushirika wasimtambue.
“Mimi niko ndani ya Kanisa, nalitambua Kanisa, namtambua Muasham Baba Askofu, Kanisa hili limesajiliwa, Kanisa la Mungu, Muasham Baba Askofu wakati nilipofika tu hapa Mkoa wa Rukwa, Sumbawanga. Pamoja na viongozi wengine waliofika ofisini wakaniombea, Baba Askofu huyu alikuja akaniombea pia, wewe ni nani usiyemtambua? Mimi niwatake na kuwaomba, wanausharika wote ambao wako nje ya Kanisa warudi ndani ya Kanisa,” Alisema.
Na kuongeza kuwa endapo waumini wakishikana Mungu huwa pamoja na waumini hao na kamwe Mungu hawezi kumfuata mtu asiyependa umoja na kuwahahakikishia kuwa wale wote ambao wapo nje ya Kanisa kuwa Baba Askofu amekwisha wasamehe hivyo wasiwe na sababu ya kuendelea kubaki nje ya Kanisa.
Ameyasema hayo aliposhiriki ibada ya ya katika kanisa la KKKT Dayosisi ya Ziwa Tanganyika Mkoani Rukwa.
Kwa upande wake Baba Askofu Ambele Mwaipopo alimshukuru Mkuu wa Mkoa huyo kwa kutoa ujumbe mzuri wa mshikamano na kuwaomba waumini waliohusdhuria ibada hiyo kuzungumza na wale wote waliopo nje ya kanisa hilo ili kuweza kuurudisha umoja na kuweza kupanga mambo ya kimaendeleo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.