Shirika la umeme TANESCO wilayani kalambo Mkoani Rukwa limewakikishia wananchi wa vijiji vilivyopo katika kata za lyowa na Matai kuwa litawapatia huduma ya umeme ndani ya mwaka huu wa 2019 kutokana na serikali kuongeza vijiji 13 kati ya 42 vilivyokuwa vimepatiwa huduma hiyo katika awamu ya tatu.
Hatua hiyo imekuja kufuatia malalamiko yaliyojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Santamaria ambapo wananchi wa kijiji cha Kisungamile kilichopo kata ya Matai wilayani kalambo mkoani hapa, walililalamikia shirika hilo kutowapelekea huduma husika licha ya vijiji vingine kuwa na umeme kwa muda mrefu sasa.
Wamesema licha ya kijiji hicho kuwa ndani ya mamlaka ya Mji mdogo wa Matai ambao ndio makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, hakina umeme na wakati huo vijiji vingine vinavyo unda mji huo vikiendelea kunufaika na huduma hiyo na kuiomba serikali kupitia shirika la umeme TANESCO kuwangalia kwa jicho la tatu.
‘’kijiji chetu ni miongoni mwa vijiji vinavyounda mji mdogo wa Matai lakini tunashangaa kuona vijiji vingine vimepatiwa tayari huduma ya umeme lakini sisi bado mpaka. Tunaliomba shirika la umeme litungalie kwa jicho la tatu ili nasisi tuweze kunufaika na huduma hii muhimu.’’Walisema wananchi hao.
Meneja wa shirika la umeme TANESCO wilayani humo Japhet Malongo amesema serikali imeongeza vijiji 13 ambavyo vitapatiwa huduma hiyo katika awamu inayoendelea hivi sasa na kijiji cha Kisungamile kikiwa miongoni na kuwataka wananchi kuendelea kuwa na subira wakati utekelezaji ukiendelea.
Mkuu wa wilaya hiyo Julieth Binyura, amewataka wananchi kuendelea kulipa fedha ya huduma kiasi cha shilingi elfu ishirini na saba na kusema lengo la serikali ni kuhakikisha kila kijiji kinapata umeme.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.