Tasisi ya kuzuia na kupambana na RushwaTAKUKURU Wilayani Kalambo mkoani Rukwa imesema haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria wasimamizi wa vituo vya kupigia kura pamoja na wagombea ambao watahusika na tuhuma za kupokea ama kutoa rushwa.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa tasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru wilayaani Kalambo mkoani Rukwa Lupakisyo Mwakyolile wakati wa zoezi la uapishaji wa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura na kuwataka kuwa waadilifu wakati wa uendeshwaji wa zoezi hilo.
Amesema uchaguzi sio suala la mzaha na kwamba maendelea ya nchi hayawezi kupatikana bila viongozi waadilifu wenye uchungu na Taifa hili. Hivyo Kamanda huyo amewataka wananchi woteWilayani Kalambo kushikamana Pamoja ili uchaguzi wa Serikali za mitaa wa tarehe 24 Novemba uwe huru na wa haki.
‘’Twendeni tukafanye kazi kwa uadilifu na kila mmoja wetu kwa nafasi yake akatimize wajibu wake. Kwa upande wetu sisi TAKUKURU hatutasita kumchukulia hatua mtu awaye yote atakayebainika kushawishi,kutoa au kupokea rushwa.’’Amesisiza Mwakyolile.
Kwa upande wake Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kalambo Erick Kayombo, amewataka wasimamizi wasaidizi ngazi zote pamoja na waandikishaji kutenda haki wakati wote wa maandalizi mpaka ukamilifu wa zoezi la kupiga kura.
‘’Tunaenda kusimamia kwa makini shughuli zote uchaguzi.Kumbukeni ndugu zangu, tukifanya vibaya kwenye uchaguzi wa Serikali mitaa tutakuwa tumevuruga na uchaguzi mkuu wa mwakani.Hivyo zingatieni sheria,taratibu na kanuni zinazo tawala suala zima la uchaguzi.’’Ameeleza Erick Kayombo Msimamizi wa uchaguzi jimbo la kalambo wakati wa kuwapicha wasimamizi wa vituo vya kupigia kura.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.