Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Wilayani Kalambo Mkoani Rukwa imekamilisha uwekaji wa matuta katika barabara za lami katika Mji mdogo wa Matai hatua itakayo saidia kupunguza ajali za barabarani.
Meneja wa TARURA Wilayani humo Mhandisi Daudi Kaigi, amesema licha ya hilo Serikali imekamilisha uwekaji wa taa za barabarani kuzunguka Mitaa ya Mji mdogo wa Matai, lengo kubwa ikiwa ni kuchochea shughuli za kiuchumi hususan biashara ndogondogo, kupendezesha Mji wa Matai na kupunguza vibaka nyakati za usiku.
Katika hatua nyingine Mhandisi Kaigi ametumia fursa hiyo kuwataka Wananchi Wilayani humo kuendelea kulinda na kutunza miundombinu ya barabara kwa kuacha kuendesha/kufanya shughuli za kibinadamu kando ya barabara ikiwemo kilimo na ufugaji.
Hata hivyo, baadhi ya watumiaji wa vyombo vya moto Wilayani humo wameipongeza Serikali kwa hatua hiyo muhimu na kuiomba kuongeza mtandao wa barabara za lami katika Mji huo ikiwemo kipande cha barabara ya kutokea Kijiji cha Singiwe.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.