Naibu waziri wa ofisi ya Rais Tamisem Deogratius Ndejembi amewaagiza waganga wakuu wa mikoa na wilaya kupanda miti ya matunda kwenye maeneo ya hosptali zote za mkoa na wilaya ili kuwawezesha akina mama wajawazito kupata matunda wakati wa kujifugua.
Ameyasema hayo kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika manispaa ya sumbawanga mkoani Rukwa uliokuwa umehusisha viongozi wa serikali na chama cha mapinduzi CCM taifa, ambapo amesema serikali imetoa fedha billion 919 ili kununua magari ya wagonjwa ambayo yatagawiwa katika Halmshauri 26 na kwamba kila halmashauri itapata gari 2 za wagonjwa.
Amesema licha ya hilo Halmashauri zote zitapata magari ya usimamizi ambapo kila Halmashauri itapata gari moja ambazo zitawawesha waganga wakuu kutembea na kukagua huduma za afya kwenye vituo vya kutolea huduma za fya.
Hata hivyo awali akiongea na wakazi wa mkoa wa Rukwa katibu mkuu wa CCM taifa Daniel Chongolo aliiagiza wizara ya kilimo kuweka utaratibu utakao wezesha kukunua mazao mengi ya wakulima kwa bei nzuri ili kukabilina na mvua za EL NINO sambamba na kulipa madeni ya wakulima ambao waliuza mazao yao NFRA bila kulipwa.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.