Wananchi wilayani Kalambo mkoani Rukwa kupitia kikao cha ushauri cha wilaya wamesema wanatamani katika dira ya mwaka 2025 hadi 2050 serikali iweke mkazo katika sekta ya afya kwa kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na kituo cha afya ikiwa ni pamoja na kila mtanzania kuwa na bima ya afya.
Wameyasema hayo kupitia kikao cha ushauri cha wilaya kilicho kuwa na lengo la kujadiri dira ya mwaka 2025 hadi 2050 na kuongozwa na katibu tawala wilayani humo Servin Ndumbalo na kusema wangetamani katika dira ya mwaka 2025 hadi 2050 sekta ya elimu ipewe kipaumbele ikiwemo kuongezwa kwa walimu ili kurahisisha swala la ujifunzaji na ufundishaji.
Richa ya hilo wamependekeza katika dira ya mwaka 2025 hadi 2050 katika sekta ya uvuvi na mifugo serikali kuweka udhibiti wa suala la ufugaji holela wa mifugo ikiwa ni pamoja na serikali kuweka Ruzuku kwenye pembejeo za kilimo ili kuwezesha wakulima kulima na kuzalisha kwa tija.
‘’Katika Sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi, matamanio yetu kufikia mwaka 2050 ni kuona serikali ikidhibiti suala la ufugaji holela, idadi ya mifugo idhibitiwe yaani kuwe na idadi ya mifugo yenye tija, wakulima wapate mbolea ya RUZUKU Kwa bei nafuu inayo wawezesha wakulima walime na wazalishe kwa ubora na wingi, pembejeo za kilimo kuboreshwa, wakulima wapewe elimu kuhusiana na shughuri nzima ya kilimo, sekta ya kilimo iwe ya kwanza kuingiza pato la Taifa, wakulima wapewe elimu juu ya urutubishaji wa ardhi mfano kilimo cha soya’’ walisema.
Richa ya hilo katika Sekta ya maji,wamesema matamanio yao kufikia mwaka 2050 wameomba serikali ifikishe huduma za maji kwa vijiji vyote vinavyo zunguka wilaya ya kalambo,pamoja na kuhamasisha jamii kutunza vyanzo vya maji.
Katika Sekta ya teknolijia na mawasiliano (mawasiliano, miundo mbinu na umeme), wamesema kufikia mwaka 2025/2050 miundo mbinu ya barabara inatakiwa iboreshwe zaidi, kwa usalama wa usafiri na usafirishaji, barabara zenye ubora na zinazo dumu muda mrefu zijengwe kwa utaalamu zaidi.
‘’Pia katika suala la tehama na mawasiliano kufika 2050 huduma za intaneti ziweze kufika hata vijijini ili kurahisisha ufanyaji kazi, mawasiliano yafike kila mahali au katika kila eneo na ya mfikie kila mmoja mfano katika maeneo ya hifadhi mawasiliano yanatakiwa yawepo, katika suala la teknolijia elimu juu ya matumizi mazuri ya teknolijia’’ walisema
Aidha katika Sekta ya uchumi (Biashara na uwekezaji) wameomba kufikia mwaka 2025/2050 suala la uwekezaji lipewe kipaumbele kwa kuwapa wananchi nafasi ya kuwekeza, elimu inayo husiana na uwekezaji itolewe kwa wanachi, kuwepo kwa viwanda vya usindikaji mfano mazao yanayo tokana na mimea na yale yanayo tokana na mifugo, viwanda vijengwe katika maeneo husika, kundi la wanawake na vijana badala ya kupewa tu mikopo (pesa) lakini pia wapewe na vifaa vitakavyo wawezesha kufanya
Wamesema katika Sekta ya Ardhi, maliasili na mazingira, matamanio yao wangetamani kufikia mwaka 2050 aridhi ipimwe kwa vipimo rasmi au maalumu Kwa ajili ya kusaidia katika ukusanyaji wa kodi, kuelimisha wananchi juu ya matumizi ya nishati safi, pia bei ya gesi inatakiwa ipunguzwe.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.