Wananchi wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameshauriwa kujenga utamaduni wa kupanga, kupima na kumilikisha maeneo yao kwa lengo la kupata hatimiliki ambazo zitawawezesha kuongeza thamani ya maeneo yao na kuondoa migogoro ya aridhi.
Hayo yamebainishwa na Afisa ardhi wilayani humo Mathayo Mvungi wakati wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia katika vijiji vya kata ya Mwimbi na kusisitiza viongozi wa serikali za vijiji kujiepusha na umilikishaji wa ardhi zaidi ya hekali 50.
Kwa upande wake mwanasheria wa halmashauri hiyo Peter Malendecha ametumia fursa hiyo kuwataka viongozi wa serikali za vijiji wilayani humo kuwa sehemu ya kuisaidia serikali katika kuwahamasisha wananchi kuingizwa kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi hatua itakayosaidia kuondoa migogoro ya wafugaji na wakulima.
Hata hivyo kampeni ya msaada wa kisheria mkoani humo imefanyika katika kata 10 zenye jumla ya vijiji 30 kwa kuwatembelea wanafunzi na wananchi kupitia mikutano ya hadhara.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.