Wananchi katika kijiji cha Kisungamile kata ya Matai wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameungana na watu wengine dunia kote katika kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji ambayo ufungunzi wake ulifanyika katika eneo la Kisumba Agost moja 2019.
Kama tunavyofahamu,kuanzia tarehe 1hadi saba Agost,kila mwaka Tanzania huungana na nchi zingine duniani kote katika kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama. Madhimisho hayo ni fulsa ya pekee katika kuunganisha nguvu za wadau mbalimbali na jamii kwa ujumla ili kiufikia malengo ya azimio la Innocenti ilililofanyika nchini Italia 1,8,1990.
Licha ya hilo kwa ujumla lengo la madhimisho ya wiki ya unyonyeshaji yamekuwa yakilenga zaidi kumnyonyesha mtoto maziwa katika saa moja ya kwanza mara tu baada ya kujifungua sambamba na kumyonyesha mtoto mra kwa mara.
Awali wakitoa elimu kwa wananchi wahudumu wa afya katika zahanati ya Kisungamile wamesema uonyonyeshaji ni jukumu la kila mtu katika nafasi yake ,watu hao ni pamoja na baba ,familia ,viongozi ,ngazi ya jamii.
Baadhi ya wananchi kijijini hapo wamesema wamenufaika na elimu iliotolewa na wahudumu wa afya na kuiomba serikali na mashirika binafus kuendelea kutoa elimu zaidi juu ya namna ya unyonyeshaji.
Hata hivyo siku za hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo alivitaka vyombo vya habari mkoani humo kufuatilia na kufanya tafiti na kuripoti juu matukiio mbalimbali ikiwemo haki ya akina mama kupata likizo ya uzazi sambamba na kutia taarifa sahihi kuhusu unyonyeshaji.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.