Hali ya taharuki na furaha imeripuka kwa wananchi wa mji wa Namanyere na viunga vyake baada ya Serikali kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujezi wa kituo cha afya cha Nkomolo na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya mungaano waTanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwaondolea adha hiyo.
Wakiongea baada ya Rais wa Jamhuri ya mungano wa Tanzania John Pombe magufuli kuzindua kituo hicho cha afya,wamesema wanauhakika kituo hicho kitawasaidia kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu wakati wa kutafuta huduma za matibabu kama ilivyokuwa hapo awali.
Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia,wazee na watoto Umi Mwalimu, amesema kituo hicho kimekamilika na kwamba mpaka sasa kinazalisha akina mama wapatao140.
‘’Mheshimiwa Rais, baada ya kufunguliwa kituo cha afya cha Nkomolo hapa mjini Namanyere, akina mama wajawazito wamehamasika kujifungulia Hospitalini ikiwa ni ongezeko chanya kutoka asilimia 72 hadi 96 kwa Wilaya nzima’’alisema waziri wa afya.
‘’Tena tumefarijiwa sana na ujio wa Madaktari kutoka Italia wanaotoa huduma za upasuaji kituoni Nkomolo ambapo hadi leo, wamefanikiwa kufanya upasuaji kwa wajawazito wenye uchungu gandamizi wapatao 166 bila kifo hata kimoja.Kwa hali hiyo Mheshimiwa Rais, nawataka Madaktari wetu wazalendo kuiga mfano huo.’’Amehimiza Umi Mwalimu.
‘’Mheshimiwa Rais, niliwahi kukuletea salamu kutoka kwa wananchi wa Wampembe wanaotembea umbali wa kilomita 130 kutoka hapa Namanyere waliokuwa wanakupongeza kwa kuwajengea kituocha afya cha kisasa’’ amesisitiza Waziri Jafo.
‘’Lakini pia sisi wasaidizi wako pamoja na watanzania wote wenye mapenzi mema wakiwemo wana Nkasi tunaendelea kufarijiwa na dhamira yako njema kimaendeleo katika Nyanja zote kwani ni mwaka jana pekee umejenga Hospitali ya Wilaya ya hapa Namanyere kwa shilingi bilioni 1.5 ikiwa ni miongoni mwa Hospitali 67 nchi nzima. Tena hujaishia hapo hata mwaka huu Serikali yako imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali 25 za Wilaya nchi nzima katika mwaka wa fedha 2019/20.’’Anafurahi na kupongeza Mheshimiwa Jafo.
Awali akiongea na hadhara ya wananchi wilayani Nkasi, Mh.Rais Wa jamhuri ya mungano Wa Tanzania John Pombe Magufuli, amesema Serikali itaendelea kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya kuimarisha miundo mbinu na kuboresha huduma za afya.
‘’Tunaendelea kuboresha huduma za afya kwa kasi. Hivi sasa tumetenga shilingi bilioni 272 kwa ajili ya kununua madawa nchi nzima ikiwemo na Wilaya ya Nkasi na vituo vyake vyote vya kutolea huduma za afya’’ Amlisema Rais Magufuli.
‘’Pia nachukua fursa hii kuwapongeza Madaktari kutoka Italia waliofika hapa Namanyere kutoa huduma ya upasuaji kwa kushirikiana na Madaktari wetu. Nipende tena kuwapongeza Madaktari na Manesi wazalendo na kwamba endeleeni kujituma na hakikisheni mnaondoa kero kwa wagonjwa’’Amesisitiza Rais Magufuli.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.