Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, Mhe.Daud Sichone amesema Halmashauri hiyo inatarajia kukusanya jumla ya shilingi bilioni 1.8 katika kipindi cha mwaka 2018/2019.
Mhe.Sichone ameyasema hayo leo katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Katika Ukumbi wa Chuo cha Maktekista kilichopo Matai wilayani Kalambo kwa lengo la kupitisha rasimu ya bajeti ya Mapato na Matumizi ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2018/2019
Akichangia katika kikao hicho Mbunge wa Kalambo Mhe.Josephat Kandege amehimizauendelezaji wa Kilimo cha zao la Mhogo pamoja na Uanzishaji wa kilimo cha zao la miwa kwa ajili ya uzalishaji wa sukari katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ili kuweza kufikia sera ya uchumi wa kati pamoja na uchumi wa viwanda.
Katika Mkutano huo Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo imetoa motisha kwa Mtendaji wa Kijiji cha Mpanga Bw. Jeophrey Sinyangwe kwa kumpatia zawadi ya pikipiki aina ya Boxer-Bajaji yenye namba za usajili MC784 BTZ ambayo ina thamani ya Shilingi Milioni mbili. Motisha hiyo imetolewa kama hamasa kwa Watendaji wenye jukumu la kukusanya mapato kutokana na Mtendaji huyo kuongoza katika ukusanyaji wa Mapato katika kipindi cha miezi sita ya mwaka wa fedha 2017/2018.
Kikao hicho kimejumuisha Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ambaye ni Katibu, Madiwani, Wakuu waIdarana Vitengo pamoja na wageni waalikwa, wananchi pamoja na Waandishi wa Habari.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.