Katika jitihada za kuwasaidia wananchi wa kijiji cha kipwa kilichopo kata ya Kasanga wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, kanisa la K.K.T Sumbawanga limetoa misaada ya vitu mbalimbali ikiwemo bati na unga ikiwa ni jitihada za kuwafariji kutokana na adha ya nyumba zao ambazo zilibomoka hivi karibuni kutokana na maji ya ziwa Tanganyika kujaa.
Hivi karibuni kulitokea mabadiliko ya tabia ya nchi katika ziwa Tanganyika kutokana na maji ya ziwa hilo kujaa na kusababisha nyumba kadhaa kubomoka katika kijiji cha kipwa na kusababisha baadhi ya familia kukosa makazi.
Kufuatia hali hiyo serikali wilayani humo ilitoa maagizo wananchi wote kuhama maeneo hayo na kuhamia maeneo ya miinuko kwa lengo la kuepukana na adha ya kupata madhara kutokanana uwepo wa maji hayo.
Mpaka hivi sasa zaidi ya kaya 40 zimehamia maeneo ya miinuko na serikali imeanza kuwasaidia kwa kulima barabara mpya kwa kiwango cha changarawe kutokea kata ya Mpombwe kuelekea kijijini hapo.
Hata hivyo mwaka 2005 kijiji cha kipwa kiliwahi kupatwa na madhara ya nyumba zao kuungua kwa moto na mwaka 2020 kilipata majanga ya maji ya ziwa Tanganyika kubomoa nyumba zao.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.