Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Rukwa imefanikiwa kuokoa fedha kiasi cha shilingi million 175.983,250/= huku milioni 56.700,000/= zikirejeshwa kwa walimu wastaafu 39 katika wilaya ya Kalambo na Nkasi ambao walikuwa wametapeliwa na chama cha UWAMI Saccos.
Akiwakabidhi fedha hizo walimu wastaafu 39 mkuu wa TAKUKURU mkoani Rukwa Hamza Mwenda mbele ya mkuu wa mkoa huo, amesema kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi million 45,315.000 \= zitarejeshwa katika acont maalm ya Benk kuu na million 56.700,000/= zitarejeshwa kwa walimu wote wastaafu waliokuwa wametapeliwa na chama hicho.
‘’walimu hawa walifika TAKUKURU na kulalamika kuwa tangu walipostaafu viongozi wa chama hicho hawajawalipa Amana zao na hawana dalili za kuwalipa na wamefuatilia kwa kipindi cha miaka minne .
Katika uchunguzi tulioufanya tulibaini kuwa uongozi wa SACCOS hiyo ulitumia akiba na hisa za wanachama wake zote kinyume na sheria ya vyama vya ushirika Na 6 ya mwaka 2013. fedha hizi tuliwabana na wamerejesha zote’.alisema Mwenda
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo , aliwasisitiza viongozi wa vyama vyote mkoani humo kuwa waadilifu kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia wanachama wao kuwaamini na kauipongeza taasisi hiyo kwa kufanya kazi nzuri ambayo imepelekea walimu hao kupata sitahiki zao.
Hata hivyo walimu wastaafu 39 wa Halmashauri ya Sumbawanga na Kalambo ambao walikuwa wanachama chama cha UWAWAMI SACCOS na viongozi wa Nkasi Techers Saccos ambacho pia ni chama Akiba na mikopo cha walimu wanao hudumu katika wilaya ya Nkasi na MAKUPA SACCOS pamoja na Halmashauri ya Sumbawanga kwa pamoja wameshiriki katika hafla hiyo ya urejeshwaji wa fedha zilizokuwa zimepotea .
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.