Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Ninga kata ya Katazi Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa amefariki dunia baada ya kupata ajari ya pikiki aliyokuwa ameipora katika eneo la Miangalua tarafa ya Laela.
Kamanda wa polisi mkoani Rukwa Justene Masejo amesema kuwa tukio hilo limetokea tarehe 17/03/2020 majira ya saa 08:30 Usiku huko kijiji cha Kamsamba kata ya Miangalua Tarafa ya Laela, Wilaya ya Laela, Mkoa wa Rukwa.
Amesema Kijana mwenye umri wa miaka 42, Mfanyabiashara, Mkazi wa Miangalua, Aitwaye Joseph Kachingwe pikipiki aina ya MC 617 CCG Kinglion, yenye thamani ya Tshs. 2,200,000/= na pesa taslimu Tshs.1,500,000/= na watu wawili ambao mmoja mpaka sasa hajafahamika.
Hata hivyo watuhumiwa hao baada ya kupora pikipiki na hizo fedha waliendesha kwa mwendo kasi na ndipo walipopata ajali na kuanguka na pikipiki hiyo ambapo mmojawapo alifariki dunia wakati anapatiwa matibabu katika kituo cha afya Laela na marehemu alijulikana kwa
jina la Steven Kalunga, miaka 29, Mkulima wa Kijiji cha Ninga Wilaya ya Kalambo.
Mhanga aliviziwa katikati ya kijiji cha Miangalua na Kamsamba barabarani kwa nyaya za umeme kisha kumpora pikipiki.
Pikipiki iliyoibiwa imepatikana na juhudi za kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Kamishna Msaidizi wa Polisi Justine Majura Masejo anatoa rai kwa wananchi wote kuwa kila mmoja awe mlinzi wa mwenzie na kuweza kudhibiti matukio ya kihalifu pamoja na wahalifu.
Aidha, anawashukuru wananchi wa kijiji cha Miangalua kwa jitihada walizozifanya kuhakikisha kuwa watuhumiwa hao wanakamatwa ingawa mmoja alifanikiwa kukimbia na juhudi za kumtafuta zinaendelea.
Halikadhalika anawataka wananchi kwa kushirikiana na wenyeviti wa mitaa pamoja na vikundi vya ulinzi shirikishi waweze kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa zinazohusiana na kuwafichua wahalifu.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.