Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa kwa kushirikiana na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Imeandaa tamasha la kutangaza utalii wa ndani linalofahamika kama KALAMBO FOREST UTALII FESTIVAL ambalo litafanyika tarehe 14 -2-2026 katika eneo la maanguko ya maji ya mto Kalambo kwa kushirikisha mashindano ya Baiskeli, kupanda ngazi ikiwa ni pamoja na kukimbia mbio fupi na ndefu.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Kalambo ambae pia ni mkuu wa Divishen ya kilimo ,mifugo na uvuvi Ndugu Nicholas Mrango, amesema mashindano hayo yanalenga kutangaza utalii wa ndani ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kutangaza utalii wa ndani ikiwemo maanguko ya maji ya mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa urefu Barani Afrika kwa mita 235.
Aidha amewataka watumishi wa umma wilayani humo kujitokeza kwa wingi kushiriki mashindano hayo ambayo yatawezesha kuimarisha afya ikiwa ni pamoja kujifunza mambo mbalimbali kuhusu utalii.
Kwa upande wake mratibu wa tamasha hilo kutoka wakala wa huduma za mistu Tanzania (TFS) ndugu Nelson Machibya amebainisha kuwa Tamasha hilo litashirikisha wananchi, watumishi wa umma kutoka taasisi mbalimbali za serikali na kwamba washiriki watapatiwa medani maalumu kutoka wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS).
Kwa upande wake kaimu mkuu wa kitengo cha utamaduni,sanaa na michezo wilayani humo ndugu Amos Mmewa, amesema tamasha hilo litahusisha ngoma za asilia pamoja na michezo mbalimbali na kwamba washiriki wote watapatiwa medani maalamu na kuvitaka vikundi mbalimbali vya sanaa na michezo kujitokeza kushiriki mashindano hayo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.