Ajali ya mlipuko wa lori la mafuta mjini Morogoro inaendelea kugharimu maisha ya watu na hivi sasa waliofariki kutokana na mkasa huo wa jumamosi asubuhi wamefikia 89.
Idadi hiyo imeongezeka baada ya majeruhi saba kati ya 32 waliokuwa wamelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuaga dunia.
Watu 62 walithibitishwa kufariki siku ya mkasa na zaidi ya 70 kujeruhiwa, na toka hapo idadi ya vifo imekuwa ikiongezeka taratibu.
Awali idadi ya majeruhi 46 walisafirishwa kutoka Morogoro mpaka Muhimbili kwa matibabu ya kibobezi, lakini mpaka saa saba mchana wa leo Alhamisi, Agosti 15 wabeaki majeruhi 25.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari wa Muhimbili, Bw Amini Aligaesha kati ya majeruhi 25 wanaoendelea kupokea matibabu, 16 wapo kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.
asilimia 80 na kuendelea.
Mkasa huo ulitokea majira ya saa mbili asubuhi ya Jumamosi baada ya lori lilibeba shehena ya petroli kuanguka katika mji wa Morogoro, na watu kuanza kuchota mafuta yaliyomwagika kisha mlipuko mkubwa kutokea.
Kumekuwa na hisia tofauti juu ya ajali hiyo lakini Rais wa nchi hiyo John Magufuli amewataka wananchi wake kuacha kuhukumu waliofariki na majeruhi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.