• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

Akina Baba Watakiwa Kuacha Tabia Ya Kunyonya Maziwa Ya Akina Mama

Posted on: August 2nd, 2019


Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda amewatahadharisha kinababa wenye tabia ya kunyonya maziwa ya kinamama wanaonyonyesha kwani hicho ni chakula maalum kwaajili ya mtoto aliyezaliwa na yeyote anayefanya hivyo anadhulumu haki ya mtoto ambaye hutegemea maziwa ya mama kwa muda wa miezi sita bila ya kula chakula cha aina yoyote.
Amesema kuwa kazi kubwa ya kinababa ni kuwawezesha kinamama kupata lishe bora ili waweze kuwa na afya thabiti kutoa maziwa ya kutosha na kuweza kuwa nyonyesha watoto wao na kuongeza kuwa katika mkoa wa Rukwa asilimia 81 ya watoto wenye umri chini ya miezi sita wanalishwa vyakula vingine vya ziada, jambo ambalo halikubaliki kwa maendeleo ya mtoto.
“Ujumbe wa Leo ni kwamba watoto wadogo chini ya Miezi Sita ndio wanaotakiwa kunyonyeshwa, kwahiyo kinababa na wao wenye kupenda maziwa ya baba waache kwasababu hicho sio chakula chao ni lishe kwa watoto wachanga, tusidhulumu haki za watoto za unyonyeshaji, tuache tabia ya kunyonya maziwa ya mama kwa wasiohusika,” Alisisitiza.

Aidha alisema kuwa tafiti zinaonesha kuwa asilimia 17 ya watoto wenye umri chini ya miezi 6 wananyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kupewa kinywaji au chakula kingine kama inavyoshauriwa na Shirika la Afya Duniani. Hii ina maana kuwa asilimia 83 ya watoto wenye umri huo hawanyonyeshwi ipasavyo.

Mh. Mtanda aliyasema hayo katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji kimkoa katika Kijiji cha Kisumba, kilichopo Wilaya ya Kalambo akimwakilisha aliyetakiwa kuwa mgeni rasmi wa uzinduzi huo Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Albinus Mgonya aliisifu timu ya afya ya Mkoa kwa kuwezesha kufanyika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji katika Kijiji cha kisumba kutokana na Kijiji hicho kuwa na kinamama wengi wanaonyonyesha.

“Katika Kijiji hiki Mheshimiwa mgeni rasmi kuna Kaya 1300, na kwa takwimu ambazo tunazo kupitia idara yetu ya afya kinamama wanaonyonyesha watoto katika Kijiji hiki cha Kisumba ni 234, hivyo utaona kwamba tumekuja kuhakikisha kuwa ujumbe huu unafika kwa wadau kwa njia muafaka,” Alieleza.

Halikadhalika alisema kuwa maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na utekelezaji wa mradi wa Lishe Endelevu unaolenga kuongeza idadi ya watoto wenye umri kati ya miezi 6 – 23 kuhakikisha kwamba wanapata vyakula vyenye mchanganyiko sahihi na kusisitiza kuwa ni muhimu kinababa kushiriki katika maadhimisho hayo ili wawe msaada mkubwa kwa kinamama.

Katibu tawaala  wilayani  humo Frank Sichalwe aliwasisitiza akinamama kuwa unyonyeshaji wa maziwa ya mama huchangia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha afya, kulinda uhai na maisha ya mtoto.

Asilimia 67 ya watoto wa umri kuanzia miezi 6 – 23 wanapewa vyakula ambavyo havina mchanganyiko wa kutosha, yaani mlo usiokamilika, hali inayodhihirisha kuwa, taratibu duni za ulishaji watoto ni mojawapo ya sababu za utapiamlo katika Mkoa wa Rukwa.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • WANAWAKE KALAMBO WAFANYA UTALI WA NDANI

    March 10, 2025
  • TALGWU YATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA

    March 10, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.