Mwenyekiti wa ALAT mkoani Rukwa Kalolo Ntila amewataka wakurugenzi kuzitumia vizuri fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo ili ziweze kuleta tija katika jamii na kusisitiza kuwekwa utaratibu maalum utakao wezesha kuanzishwa miradi itakayo jengwa kwa kutumia fedha za mapato ya ndani.
Ameyasema hayo kupitia kikao cha ALAT kilichofanyika kwa ngazi ya mkoa katika halmashauri ya kalambo mkoani Rukwa na kuwataka wakurugenzi mkoani humo kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ikiwemo kuanzisha vyanzo vipya vya mapato ili kufikia malengo ya serikali katika ukamilishaji wa miradi ya maendeleo.
Mapema wakiongea kupitia kikao hicho mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kalambo Shafi Mpenda amesema katika mwaka wa fedha 2023/2024 hadi kufikia tarehe 15/4/2024 halmashauri ilipokea fedha kiasi cha shilingi 5,780,828,450,63 kutoka serikali kuu kupitia fedha za ndani na nje kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo miradi ya afya na utawala .
Aidha amesema hadi kufikia mwezi machi 2024 pekee halmashauri imetumia kiasi cha Tshs 133,159,359,305 .00 kwenye miradi ya maendeleo na kufanya jumla ya matumizi kuanzia julai 2023 hadi machi 2024 kuwa Tshs 4,959,853,548,74 sawa na asilimia 46
kwa upande wake kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga KulaNGA Kanyanga ,amesema halmashauri ya manispaa hiyo imefanikiwa kusambaza madawa na vifaa tiba katika zahanati 28 vituo vya afya na hospitali ya wilaya ikiwa ni pamoja na kukamilisha miundombinu mipya ya kutolea huduma katika shule za msingi na sekondari.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.