ASKOFU wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Ambele Mwaipopo amewaomba wananchi wa mikoa ya Rukwa na Katavi, kumpigia kura za Kishindo Rais Dkt. John Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao ili ashinde kipindi kingine cha miaka mitano ambacho kitamuwezesha kukamilisha miradi ya kimkakati aliyoianzisha tangu aingie madarakani.
Akizungumza na vyombo vya habari hivi karibunii,Askofu Mwaipopo alisema yeye binafsi amelazimika kutoa ombi hilo kutokana na kuvutiwa na utendaji kazi wa Rais Magufuli pamoja na kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika uongozi wake, kitendo kinacho sababisha afanikishe maono yake pamoja kuiwezesha nchi kupiga hatua za maendeleo.
Alisema kuwa pia kitendo cha kufanikiwa kutekeleza miradi hiyo mikubwa ndiyo iliyosababisha mpaka Benki ya dunia kuamua kuitangaza nchi ya Tanzania kuwa imeingia katika kipato cha kati hali ambayo Watanzania watapata maendeleo makubwa kupitia miradi hiyo.
Askofu huyo alisema kuwa lengo lilikuwa nchi iingie katika uchumi wa kati mwaka 2025 lakini kwa ajabu na muujiza wa Mwenyezi Mungu imechukua miaka minne na nusu kufikia lengo badala ya miaka kumi kama ilivyotarajiwa hapo awali inaonekana mafanikio hayo yamefikiwa kwakuwa Mungu ametaka kumtunukia zawadi hii rais Magufuli akiwa bado madarakani na si baada ya kuondoka katika madarakani.
‘’Tunapoelekea katika uchaguzi mkuu mwezi Oktoba, tusiache na sisi mioyo yetu kumdondokea Rais Dkt. Magufuli kwa kumpigia kura za kishindo ili aendelee kutuongoza kwa kipindi kingine,na kumpigia kura itakuwa ni sehemeu ya shukrani zetu Watanzania kwa Mungu kutujalia Rais anaye tudondoshea moyo wake kwa kutupenda’’ alisema askofu Mwaipopo.
Alisema kuwa vile vile tunapaswa kumchagulia Wabunge na Madiwani wazalendo,wachapakazi,waadilifu na waaminifu watakao tanguliza maslahi ya taifa na si maslahi yao binafsi ili mwisho wa yote, nchi iwe kinara cha mafanikio na kuendelea kuwa mfano wa kuigwa.
Hata hivyo ametumia fusra hiyo kuwapongeza Makamu wa Rais Samia Suluhu,Waziri mkuu Kassim Majaliwa,mawaziri wabunge, madiwani na wananchi wote kwa kufanya kazi kwa bidii huku wakipewa ari na kauli mbiu ya hapa kazi tu hatua iliyosababisha nchi kuingia katika uchumi wa kati.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.