Baraza la kilimo la Taifa Tanzania kwa kushirikiana na shirika la USAID limekabidhi msaada wa vitendekea kazi kwa vijana wilayani Kalambo mkoani Rukwa ikiwemo mtambo wa kuchakata mahindi mashambani pamoja na pikipiki moja ambavyo vitawawezesha vijana kulima na kuzalisha kwa tija.
Msaada huo wenye thamani ya 4000 dollors za Kimarekani umekibidhiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kalambo Daud Sichone kupitia hafla iliofanyika katika Ofisi za Mkurugezi Mtendaji Halmashauri ya Kalambo na kushuhudiwa na Afisa Mradi kutoka Baraza la Kilimo Tanzania Bi.Beth Musa na kumkabidhi Moses Simuyemba mkazi wa Kijiji cha Ilambila wilayani Kalambo.
Mwenyekiti wa Halmashauri Daudi Sichone amesema lengo la Serikali ni kuwawezesha vijana kiuchumi na kusisitiza vijana kufanya kazi kwa bidhii ikiwemo kujikita kwenye shughuli za uzalishaji hasa katika Kilimo ili kuendelea kunufaika na miradi ya serikali na hatimaye kufikia malengo yao.
Kaimu mkurugenzi mtendaji Halamashauri ya Kalambo Erasto Mwasanga, amesema lengo la serikali ni kuwafikia vijana wote na kusisitiza mashirika mengine kuendelea kujitokeza katika kuwawezesha vijana ikiwemo kutoa vifa mbalimbali ili kuwawezesha kunufaika na kilimo.
Baadhi ya mandiwani wilayani akiwepo piter Simuyemba, ambao licha ya kuipongeza serikali kwa kutoa misaada hiyo wakamtaka mnufaika wa mradi huo kuvitumia vifaa hivyo katika kuwawezesha vijana wengine kupata ajira na kuvitumia vifaa hivyo kulingana na malengo ya serikali.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.