Zaidi ya shilingi billion 35 zimetolewa na serikali kwa ajili ya umaliziaji wa barabara kwa kiwango cha lami km 25 itakayo unganisha kati ya nchi ya Zambia na Tanzania kuanzia kijiji cha Tatanda hadi hadi mpaka wa Kasesya wilayani Kalambo mkoani Rukwa
Mkuu wa wilaya ya Kalambo Lazaro Komba kupitia mikutano ya hadhara iliofanyika katika vijiji vya Tatanda, Katete na Kaluko iliokuwa na lengo la kutoa elimu kwa wananchi watakao pitiwa na mradi huo ,amesema kwa kuona umihimu wa barabara hiyo serikali imetoa fedha zaidi ya billion 35 zitakazo wezesha kumalizia kipande cha barabara hiyo na kuwataka wananchi kuunga mkono jitihada za serikali kwa kutoa ushirikiano pindi mradi huo utakapo anza kutekeleza.
Kwa upande wake Mthamani wa mkoa wa huo Berin Mushi amebainisha kuwa watu watakao lipwa ni wale watakao pitiwa na mradi huo ambapo kwa upande wa mashamba kwa hekali moja serikali italipa shilingi laki tano kwa maeneo ya vijijini na laki nane kwa watu wanaoishi maeneo ya mpaka wa kasesya.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.